Wanafunzi wa kike wa Madrasa ya Hazrat Zaynab (a.s.), Kigamboni, Dar es Salaam, walifanya safari ya siku moja ya mapumziko katika kituo cha burudani cha Fun City tarehe 15 Juni 2026, ambapo walishiriki michezo mbalimbali, kula pamoja na kuswali Swala za Adhuhuri na Alasiri, kwa lengo la kurefresh akili, kuimarisha mshikamano na kujenga afya ya kiakili na kimwili.
Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Wanafunzi wa kike wa Madrasa ya Hazrat Zaynab (a.s.), Kigamboni, jijini Dar es Salaam, walifanya safari maalumu ya mapumziko na kuburudisha akili (refreshment trip) katika kituo cha burudani cha Fun City siku ya Jumatatu, tarehe 15 Juni 2026.
Safari hiyo ya siku moja ililenga kuwapa wanafunzi fursa ya kupumzika baada ya kipindi cha masomo na mitihani, kuimarisha mshikamano wao na kurejesha nguvu za kiakili na kimwili kupitia michezo na burudani mbalimbali katika mazingira salama na yenye maadili.
Katika safari hiyo, wanafunzi walishiriki michezo tofauti ikiwemo kuogelea, mpira wa wavu na michezo mingine ya burudani, hali iliyowafanya kufurahia siku hiyo kwa shangwe na furaha kubwa. Aidha, walipata chakula cha mchana pamoja katika eneo hilo na kutekeleza Swala za Adhuhuri na Alasiri kwa pamoja, wakidumisha maadili ya Kiislamu sambamba na shughuli za mapumziko.
Uongozi wa madrasa ulieleza kuwa shughuli za aina hii ni sehemu ya malezi kamili ya mwanafunzi, kwani pamoja na elimu ya darasani, zinachangia afya ya akili, kuimarisha udugu, ushirikiano na kujenga mazingira mazuri ya kujifunza.
Safari hiyo ilihitimishwa kwa wanafunzi kurejea salama wakiwa na kumbukumbu nzuri, furaha na hamasa mpya ya kuendelea na masomo yao.
Your Comment